Watu 10 wamefariki dunia na wengine
33 kujeruhiwa katika ajali mbaya iliyohusisha magari matatu katika
eneo la Mkata kijiji cha Mbweni Wilayani Handeni Mkoani Tanga nchini
Tanzania.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama
Barabara mkoa wa Tanga amesema kuwa ajali hiyo imehusisha mabasi
mawili ya abiria na gari dogo ambalo lilikua likitaka kulipita roli
lililokua mbele yake na ndipo ilipogongana uso kwa uso na basi la
Ratco kisha basi hilo lilipopoteza muelekeo na kugongana na basi
jingine la abiria la Ngorika.
Askari wa usalama barabarani wakichunguza ndani ya basi lililoanguka




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni