Mtanzania anayehusishwa na tukio la
shambulio la kigaidi la Chuo Kikuu cha Garissa lililouwa wanafunzi
148, ataendelea kushikiliwa kizuizini na jeshi la polisi Kenya kwa
muda wa mwezi mmoja.
Mahakama moja Jijini Nairobi leo
imeagiza mtanzania huyo Rashid Charles Mberesero almaarufu kama
Rehani Dida, atashikiliwa pamoja na watuhumiwa wenzake watano wa
shambulio hilo.
Siku ya jumanne Mberesero hakuwepo
mahakamani kutokana na kusafiri kwenda Garissa akiwa na wapelelezi
wanaochunguza shambulio hilo, wakati mahakama ikitoa amri kwa
watuhumiwa 14 wanaodaiwa kuwa ni wa kundi la al-Shabaab wakiswekwa
rumande kwa muda wa siku 30 wakisubiri uchunguzi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni