Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani
John Kerry ameionya Iran kuhusiana na tuhuma za kuhusika kuwaunga
mkono waasi wa Shia Houthi nchini Yemen.
Amesema Marekani itaungana na nchi
yeyote ya Mashariki ya Kati ambayo itahisi kutishiwa na Iran, na
kuongeza kuwa Marekani haitokaa kimya ikiona Iran inaleta machafuko
katika ukanda huo.
Marekani imeongeza hatua ya kuunga
mkono muungano unaoongozwa na Saudi Arabia kukabiliana na waasi wa
Houthi, ambao wamemtimua rais wa Yemen nje ya nchi hiyo.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni