Mwanaume anayetuhumiwa kuhusika na
tukio la mabomo katika mbio za marathoni za Boston mwaka 2013,
amekutwa na hatia ya mashtaka yote 30 yanayomkabili ambayo yanaweza
kumfanya akabiliwe na adhabu ya kifo.
Jopo la wazee wa mahakama ya
Massachusetts, wataamua iwapo mtuhumiwa huyo Dzhokhar Tsarnaev,
atapatiwa adhabu ya aina gani.
Watu watatu walikufa na wengine
zaidi ya 260 wamejeruhiwa wakati mabomu yalipolipuka katika eneo la
kumalizia mbio za marathoni Aprili 2013.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni