Takwimu za Utafiti wa Afya
zinaonyesha mwanaume mmoja kati ya kumi nchini Kenya amepatwa na
tukio la kupigwa ama kudhalilishwa kijinsia na mkewe ama mpenzi wake
wa kike.
Katika takwimu hizo wanaume wenye
umri wa miaka 20 na 24 Kenya wanakabiliwa na asilimia 11.7 ya
kufanyiwa ukatili na wanawake, wakifuatiwa kwa karibu na wanaume
wenye umri wa miaka 40 na 49 kwa asilimia 9.8.
Kwa wanaume wenye umri wa miaka 30
na 39 kumeripotiwa kuwa na matukio machache ya kupigwa na wanawake
kwa asilimia 7.1, kwa mujibu wa utafiti huo wa mwaka 2014.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni