Watu 10 wamefariki dunia, tisa kati yao wakifariki papo hapo na mwingine mmoja akipoteza maisha akiwa njiani akipelekwa hospitali kwa matibabu huku wengine zaidi ya 50 wakijeruhiwa, baada ya basi la Unique kugongana na lori la kampuni ya Coca Cola katika barabara kuu ya Shinyanga - Nzega.
Basi hilo lenye namba za usajili T 148 BKK aina ya Scania lilikuwa linatoka mkoani Mwanza kuelekea mkoani Tabora.
Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa, ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa lori hilo lililokuwa linavuta tela kujaribu kulipita gari jingine, lakini kabla tela halijarudi sawa eneo lake, lilikutana na basi hilo lililokuwa katika mwendo kasi.
Wananchi wakijaribu kutoa msaada baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni