Inaonekana mbunifu wa mavazi, modo,
rapa na muigizaji Amber Rose na mumewe rapa Wiz Khalifa wanaweza
kumaliza tofauti zao kwa ajili ya manufaa ya mtoto wao ambaye
walikuwa wakigombea kumlea.
Amber Rose ametumia Instagram yake
kutoa ujumbe mzito wa mahaba kwa mumewe huyo mtata akisema kuwa Wiz
Khalifa ndiye mpenzi wa maisha yake.
Amber aliyeomba talaka mwezi
Septemba ikiwa ni chini ya mwaka mmoja tu tangu waoane, lakini sasa
ameonyesha kubadili moyo wake kutokana na kusema hamna mwanaume
anayemfanya awe na furaha kama Wiz Khalifa.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni