Baharia mmoja wa Marekani ameishi
kwa miezi miwili baharini baada ya kupotea huku akiishi kwa kula
samaki wabichi na kunywa maji ya mvua.
Baharia huyo Louis Jordan mwenye
umri wa miaka 37, alipatikana na meli ya Ujerumani iliyokuwa ikipita
umbali wa maili 200 kutoka pwani ya North Carolina siku ya Alhamisi.
Baharia huyo alipotea baharini baada
ya boti lake la futi 35, kupinduliwa na mawimbi, ambapo Jordan
alikutwa ameka juu ya boti hilo lililopinduka juu chini.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni