Miili ya watu wanne imepatikana
kutoka katika kifusi baada jengo la ghorofa sita kuanguka likiwa bado
lipo katika ujenzi katika eneo la Roysambu Jijini Nairobi nchini
Kenya.
Watu wengine sita wamelazwa katika
hospitali ya jirani na eneo hilo ya Neema Hospital, huku wengine
watatu wakihamishiwa katika hospitali ya taifa ya Kenyatta.
Wakati jengo hilo likianguka
lilikuwa na mafundi 15 wakiendelea na ujenzi, ambapo hadi sasa
mafundi 6 hawajulikani walipo na huenda wamekwama kwenye vifusi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni