Rais Barack Obama amepongeza mpango
wa makubaliano ya kuizuia Iran kuendelea na programu yake ya nyuklia,
kuwa ni wa kihistoria, na iwapo utatekelezwa kwa vitendo utaifanya
dunia kuwa salama.
Mpango wa utekelezaji wa makubaliano
hayo umefikiwa baada ya mazungumzo ya kina, yenye lengo la kuizuia
Iran kutengeneza silaha za nyuklia ili iondolewe vikwazo
ilivyowekewa.
Irani na mataifa sita yenye nguvu
duniani yaliyohusika katika mazungumzo hayo sasa yanangojea hatua ya
kukamilisha mpango huo.
Raia wa Iran wamekuwa wakisherehekea
mitaani mpango huo, lakini kwa upande wake Israeli imesema
makubaliano hayo yanatishia uwepo wa Israeli.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni