Balozi
wa kudumu wa Umoja wa Afrika, Mhe. Amina Salum Ali leo ametoa salamu za
rambi rambi kwa Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita aliyefariki siku
ya siku ya Jumapili April 26, 2015 asubuhi na kuzikwa siku ya Jumanne
April 28, 2015 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Balozi Amina Salum Ali alisema
amepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa za kifo cha mmoja wa
watumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (TPDF), aliendelea kwa kusema Brigedia Jenerali msataafu Hashim
Mbita atakumbukwa Tanzania, bara nzima la Afrika na dunia kwa jumla
kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji
wa utawala wa ukoloni barani Afrika, hususan utawala wa kidhalimu wa
makaburu Zimbabwe na Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa
aliyekuwa Rais mzawa wa kwanza nchini Afrika Kusini, hayati Nelson
Mandela.
Mzee Mbita
alijitoa mhanga kuongoza mapambano ya ukombozi wa Afrika, Atakumbukwa
milele kwa kurudisha heshima ya Muafrika.
Brigedia
Jenerali msataafu Hashim Mbita ni mfano uliotukuka kwa watanzania na
Afrika.Aliiongoza vizuri sana kamati ya ukombozi ya Umoja wa Afrika
Mungu amlaze pema peponi, Amin.
Balozi Amina Salum Ali yupo safarini kuelekea Tanzania.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni