Basi la timu ya
Fenerbahce limeshambuliwa na mtu mwenye silaha baada ya mchezo wa
Ligi Kuu ya Uturuki ambao walishifunga Rizespo kwa mabao 5-1.
Dereva wa vinara hao wa
ligi amekimbizwa hospitali, hata hivyo hakuna hata mchezaji mmoja wa
Fenerbahce aliyeumia katika shambulio hilo lililotokea wakati
wakielekea katika uwanja wa ndege wa Trabzon.
Waziri Mkuu wa Uturuki
Ahmet Davutoglu amesema uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea.
Shirikisho la Soka la
Uturuki limelaani shambulio hilo, naye Katibu Mkuu wa timu ya
Fenerbahce, Mahmut Uslu amesema tukio hilo ni jambo lisilofaa.
Mchezaji wa Fenerbahce akitoa macho asiamini kilichotokea



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni