Timu ya Arsenal jana
imeichakaza Liverpool kwa mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya
Uingereza uliochezwa kwenye dimba la Emirates.
Katika mchezo huo mabao
ya Arsenal yalipachikwa kimiani na Hector Bellerin, Mesut Ozil,
pamoja na Alexis Sanchez na kuharibu kabisa mahesabu ya Liverpool
kuingia katika nafasi ya nne bora.
Kipa wa Liverpool akijaribu kuzuia mpira usiingie langoni
Raheem Sterling ni kama akiashiria kipigo kinatosha
Nayo Manchester United
iliifunga Aston Villa mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa katika Dimba
la Old Traford, ambapo Wayne Rooney alifunga bao la kiufundi, wakati
kiungo Ander Herrera akipachika mawili. Bao pekee la Villa lilifungwa
na Christian Benteke.
Wayne Rooney akijipinda kufunga goli lake la ajabu
Na goli la ajabu la
Charlie Adam alilolifunga kutoka umbali wa yadi 66 litabakia
katika historia ya soko licha ya Chelsea kuifunga Stole mabao 2-1
katika dimba la Stamford Bridge.
Katika mchezo huo Eden
Hazard alipachika kimiani bao la kwanza baada ya Cesc Fabregas
kuwekwa chini katika eneo la penalti na Loic Remy alikamilisha
ushindi wa Chelsea kufuatia makosa ya kipa wa Stoke, Asmir Begovic.







Hakuna maoni :
Chapisha Maoni