.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 29 Aprili 2015

BORUSSIA DORTUMND YAITUPA NJE BAYERN MUNICH KOMBE LA UJERUMANI

Timu ya soka ya Bayern Munich imeshindwa katika harakati zake za kuendelea kukusanya vikombe nchini Ujerumani, baada ya kushuhudia usiku wa kuamkia leo ikitupwa nje ya kombe la Ujerumani na Borussia Dortmund katika mchezo wa nusu fainali ya kombe hilo uliomalizika kwa mshindi kupatikana kwa mikwaju ya penati. 

Dakika 90 zilishuhudia timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, bao la Bayern Munich likifungwa na Lewandowski katika dakika ya 29 kipindi cha kwanza, bao lililodumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika. 

Kipindi cha pili Borussia Dortmund walisawazisha bao hilo kupitia kwa Aubameyang katika dakika ya 75. 

Katika upigaji wa penati, Bayern Munich ilishuhudia ikikosea penati nne na Borussia Dortmund ikitumbukiza penati mbili hivyo kufuzu kucheza fainali ya kombe hilo. 

Pamoja na kushindwa kufuzu kwa hatua ya fainali ya kombe la Ujerumani, Bayern Munich tayari ni mabingwa wa ligi kuu nchini humo msimu huu.Kocha mkuu wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp akishangilia baada ya timu yake kupata tiketi ya kucheza fainali ya kombe la Ujerumani.
Wachezaji wa Borussia Dortmund wakifurahia kufuzu kucheza fainali ya kombe la Ujerumani baada ya kuifunga Bayern Munich kwa mikwaju ya penati usiku wa kuamkia leo.





Hakuna maoni :

Chapisha Maoni