Jumatano, 29 Aprili 2015
BRIGEDIA JENERALI ( MSTAAFU ) HASHIM MBITA AZIKWA LEO KWENYE MAKABURI YA KISUTU, JIJINI DAR
Viongozi mbali mbali wa Dini ya Kiislam wakishiriki pamoja na waumini wao kwenye Ibada ya kuuswalia mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo na baadae kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo.Picha zote na Hamis Makuka.
Maelfu ya waunini wa kiislam wakishiriki kuubeba mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita wakati wakiutoa kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo na tayari kwa kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ya Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakiongoza shughuli ya kuusafirisha mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita kuelekea kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo
Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali (Mstaafu) Hashim Mbita, ambaye amezikwa kwa heshima zote za kijeshi na kwa taratibu ya dini ya Kiislam kwenye Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo
Mwili umewasili makaburuni tayari kwa Mazishi.
Shuguli na taratibu zote za Mazishi zikiendelea.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo Kaburini.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange akiweka udongo Kaburini.
Viongozi mbali mbali walioshiriki kwenye Mazishi ya Marehemu Brigedia Jenerali (Mstaafu) Hashim Mbita. Kwa hisani ya Michuzi Blog
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni