Aliyepata kuwa mkuu wa mikoa mbalimbali nchini, Mzee Chrisant Majiyatanga Mzindakaya ( mwenye koti ) akimkabidhi msaada mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mh Elasto Mbwilo kwa ajili ya waathirika wa mafuriko katika kijiji cha Lamadi wilayani Busega. Kulia ni mkuu wa wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mh Elasto Mbwilo akimkabidhi msaada aliopokea toka kwa Mzee Chrisant Majiyatanga Mzindakaya, mkuu wa wilaya ya Busega Paul Mzindakaya ( mwenye kaunda suti nyeusi )
Mkuu wa wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya akimkabidhi msaada huo diwani wa kata ya Lamadi
Mzee Chrisant Mzindakaya akisikiliza kwa makini mara baada ya kufika kijiji cha Lamadi kukabidhi msaada baada ya mafuriko kuyakumba kijiji hicho na kuwaathiri wananchi wengi hivi karibuni.
Na Shushu Joel,Busega.
Aliyewa kuwa kiongozi wa nchi hii kwa muda mrefu katika nyadhifa mbalimbali ukiwemo uwaziri wa viwanda na ukuu wa mkoa Chrisant Maji ya Tanga Mzindakaya amewapa pole wanakijiji cha Lamadi kwa kukumbwa na mafuriko.
Majiyatanga ameyasema hayo jana alipokuwa akikabidhi msaada wa fedha taslimu milioni tatu kwa waathirika wa mafuriko katika kijiji cha lamadi wilayani Busega katika mkoa wa Simiyu yaliyotokea wiki mbili zilizopita.
Aidha Majiyatanga alisema kuwa ameguswa sana na mafuriko ya ndugu zake na ndio maana amekuja kutoa chochote ili kiweze kuwasaidia kwani hali kama hizi zinakuja bila maandalizi hivyo akawapa pole sana wote waliopatwa na mkasi huu na mungu atawasaidia.
Mbali na hayo alisema " napongeza Dk Kaman kwa uongozi wake na kuwasihi wasukuma kiongozi wenu ni mzuri na kaeni mkiamini atawafikisha mbali kimaendeleo kwani namfahau" alisema .
Akipokea msaada huo Mkuu wa mkoa Elaston Mbwilo alimpongeza Maji ya Tanga na kusema kuwa ni moja kati ya viongozi wanaofaa kuigwa katika nchi hii kwani wamekuwa na mchango mkubwa kwa taifa letu.
Mbwilo aliwataka viongozi wengine kufuata nyayo za mzee huyo ambaye amefika busega kujitolea msaada kwa ajili ya waathirika wa mafuriko ambao mpaka sasa watu 1686 hawana makazi kutokana na mvua kubwa kubomoa nyumba zao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya maafa ya wilaya ambaye pia ni mkuu wa wilaya Paul Mzindakaya mtoto wa mwanasiasa huyo mkongwe alimpongeza Baba yake na kumshukuru kwa msaada huo alioutoa kwa watu wake wa Busega.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni