Jeshi la polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu tisa ( 9 ) waliokuwa wamejifungia ndani katika msikiti wa Sunni eneo la Kidatu wilayani Kilombero wakiwa na silaha za aina mbalimbali pamoja vifaa vya milipuko.
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Leonard Paul amesema katika operesheni kabambe ya kuwakamata watuhumiwa hao, askari mmoja alijeruhiwa kwa kukatwa shingo na jambia.
Kamanda huyo amesema kukamatwa kwa watu hao kumefanikiwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
Watu hao wanashikiliwa kwa mahojiano, na Kamanda Paul amesema hawezi kutaja majina yao kwa muda huu mpaka hapo upelelezi utakapokamilika.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
.jpg)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni