Cristiano Ronaldo amefunga goli la
300 akiwa na klabu ya Real Madrid na kuwa mchezaji wa tatu wa klabu
hiyo kufikisha idadi hiyo ya magoli na kuungana na wachezaji Alfredo
Di Stefano na Raul.
Mshambuliaji huyo raia wa Ureno
alipachika bao dhidi ya Rayo Vallecano katika dakika ya 68 na
kuifanya Real kuwa nyuma kwa pointi nne dhidi ya vinara Barcelona,
licha ya kupewa kadi kimakosa kwa kujirusha jambo litakalomfanya
akose mchezo wa La Liga dhidi ya Eibar.
Mbali na hilo Ronaldo sasa
amefikisha mabao 300 katika michezo 288 akiwa na Real na kufanya kile
ambacho mshambuliaji anapaswa kufanya, kwa kupiga mpira wa kichwa kwa
chini na kumpita golikipa Cristian Alvarez.
Ronaldo akianguka chini katika tukio analodaiwa kujirusha
Ronaldo badala ya kupewa penati alilambwa kadi na refa



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni