.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 27 Aprili 2015

DK KAMAN AENDESHA HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA SHULE YA MSINGI BULIMA B




                                                                                             Na Shushu Joel,Busega

WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Busega Dk Titus Kaman amewapa somo wananchi wa kata mpya ya Nyashimo juu ya umuhimu wa elimu.

Maneno hayo ameyasema wakati akiendesha harambee ya ujenzi wa shule ya msingi Bulima B ambayo bado haijakamilika na wanafunzi wake wanasomea katika shule ya jirani ya nNashimo iliyoko kata hiyo.

Kamani amewapongeza wananchi hao kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wao kwa kuchangia elimu,akitolea mifano kwa baadhi ya makabila hapa nchini ambao wao tayari awawazii tena masuala ya ujenzi wa shule bali ni katika maendeleo mengine, mikoa hiyo ni Kilimanjaro,Mbeya na Kagera

Pia Kaman aliongeza kuwa sisi wasukuma tunanafasi kubwa sana ya kusonga mbele kimaendeleo kuliko mikoa mingine hapa nchini na hii ni kwa sababu kuwa sisi tuko wengi na tunavitega uchumi vingi kuliko wao kwani hata wataalam wanasema kuwa mtoto anayekunywa maziwa na kula samaki anakuwa na akili sana.

Pia Kaman amewashangaa sana wanabusega wanaoishi nje ya Busega kwa kuchangia kiasi kidogo kuliko wazazi wao wanaoishi katika mazingira magumu huku nyumbani na huku wao wanakula vizuri ila kama wangekuwa wenzetu wa makabila mengine basi ingekuwa ni mabilioni ya pesa, ni lazima tuwe na uchungu na elimu pia tujitume na kuongeza bidii katika kuhakikisha kule tulikotoka panakuwa pa mfano kimaendeleo.

Aidha Kaman amewaasa wazazi kuhakikisha kuwa watoto wote wanapata elimu kwani elimu ni msingi wa maisha na pia mkumbuke kuwa kipindi hili si cha miaka ya mababu zetu ya mtoto kulithi mashamba,majumba na vitu vingine bali ulithi wa uhakika kwa mtoto wa leo ni elimu alisema Kaman.

Harambee hiyo iliwakutanisha watu mbalimbali akiwemo kaimu mkurugenzi wa Halmashaul hiyo ya Busega Gaudencia Bamugileki ambaye alimwagia sifa waziri Kaman kwa jitihada zake za kijitoa kwa dhati katika shughuli za maendeleo katika wilaya hiyo.

Bamugileki alimuhakikishia waziri Kaman kuwa wao kama halmashaul watahakikisha ifikapo mwezi wa saba wanafunzi watakuwa wamesha rudi katika shule yao na kuendelea na masomo kama kawaida.

Kwa upande wa wananchi wa kijiji cha Bulima wakiongozwa na Afisa mtendaji wa kata hiyo Mathias mahema walisema kuwa wanampongeza waziri Kaman kwa msaada wake wa mabati 100 ya futi kumi.

Kahema aliongeza kuwa kwa nguzu za kamani tumeweza kupata mifuko ya saruji 275,mabati105 na pesa tasilimu million 14 na kuahidi kuwa kwa mwanzo huu lazima shule ijengwe na wanafunzi wasome na kuondokana na shida ya kuvuka barabara kuu.

mwisho

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni