.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 27 Aprili 2015

EDEN HAZARD ATWAA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA WA ENGLAND

Mshambuliaji mahiri wa timu ya soka ya Chelsea, Eden Hazard amechaguliwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka wa England na kutwa tuzo ya PFA.

Mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji mwenye miaka 24, ameshatumbukiza mabao 18 mpaka sasa, na ameisaidia timu yake kutwaa kombe la Capital One. 

Pia ni mmoja wa wachezaji ambao wamekuwa na msaada mkubwa kwa Chelsea inayopigania ubingwa wa msimu huu.
Naye mchezaji wa Tottenham, Harry Kane ametwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi. Kane mwenye miaka 21 amekuwa katika kiwango cha hali ya juu akiwa na timu yake inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza.
Ji So-Yun wa Chelsea akiwa na tuzo yake baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora kwa upande wa wanawake.
Leah Williamson wa Arsenal akiwa na tuzo yake baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora chipukizi wanawake wa mwaka wa PFA.



Hakuna maoni :

Chapisha Maoni