Moja ya magari yaliyobeba misaada mbalimbali
Na Shushu Joel,Busega
MBUNGE wa jimbo la Busega na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kaman ametoa misaada mbalimbali kwa ajili ya wahanga wa mafuriko katika kijiji cha lamadi wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo, Dk Kaman amewataka wakazi wa lamadi kuwa wapole katika kipindi hiki kigumu sana kwani wengi Hawana pa kuishi na hii ni kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na inayoendelea kunyesha katika wilaya hiyo.
Misaada aliyoitoa Dk Kaman kwa wahanga hao ni unga tani 2,Mchele kg 700, Mablanketi 2500,maji ya kunywa katoni 90,maharangwe kg 800,sukali kg 600 na chumvi mifuko 200.
Akiwakabidhi misaada hiyo, aliambiwa kuwa na subira kwani timu iliyoundwa ikimaliza kufanya kazi yake ya kuratibu viizuri wale wote watakaobainika watapata msaada mwingine, ila huu ni wa kuanzia kwa kipindi hiki ambacho hali bado ni tete.
"Nimeguswa na tukio hili na ndio maana nimekuja haraka sana kuwaona na kuwapatia misaada hii ili muweze kusongeshe maisha mbele katika maendeleo ndani, alisema Dk Kaman.
Kwa upande wa mmoja wapo waliopokea misaada hiyo Rebeka Holoo mkazi wa kitongoji cha mwalukonge kijiji cha Lamadi amesema kuwa anampongeza Dk Kaman kwa misaada yake yote ndani ya lamadi na kudai kuwa ni viongozi wachache wanaoweza wakafanya kama hayo.
Ally Ntemi yeye anaishi na familia ya watu 7 katika kitongoji cha kisesa wilayani humo amesema kuwa Dk Kaman ni sawa na Obama katika utendaji na ufanisi wa kazi.
Ntemi alisema kuwa kwa mda wa siku chache familia yake ilikuwa na mahindi na Mtama, lakini mara baada ya mvua hiyo kunyesha na mafuriko yote yalisombwa na maji, hivyo anashukuru kwa msaada huo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni