Serikali ya Kenya imeagiza kufungwa
kwa kampuni 13 za kuhamisha fedha ili kuzuia vikundi vya wapiganaji
wa Kiislam kutotumia kutuma fedha za kufanya mashambulio ya kigaidi.
Waziri wa Mambo ya Ndani Joseph
Nkaissery pia amesema Kenya imefunga akaunti za benki 86 za watu
binafsi pamoja na mali zao kushikiliwa.
Hatua hizo zinaaminika kuilenga
kampuni ya mabasi na hoteli inayodaiwa kuwa na uhusiano na kampuni ya
nchini Somalia.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni