Na Shushu Joel wa Rweyunga Blog, Busega.
WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Busega Dk Titus Kaman ametembelea chanzo cha mafuriko katika kijiji cha Lutubiga wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
Amezungumza na wananchi wa kijiji cha Lutubiga ambako ndiko mafuriko yalianzia kutokana na bwawa kuzidiwa maji na kisha maji hayo kuanza kupita juu na kuelekea katika vijiji vya jirani vya lamadi na hivyo kusababisha madhara makubwa kwa wakazi hao.
Dk Kaman aliwapa pole wakazi wa maeneo hayo na kuwasihi kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu kwao na hii ni kutokana na nyumba za wananchi zipatazo 288 kubomoka na kufanya jumla ya wakazi 1686 kukosa makazi ya kuishi.
Hivyo Dk Kaman aliitaka kamati iliyoundwa kushughulikia na kutambua wahanga iweze kufanya kazi hiyo haraka iwezekanavyo ili kuweza kuwasaidia wale wote waliokumbwana mafuriko hayo.
Kwa upande wake msimamizi wa bwawa hilo linalodaiwa kuwa ndicho chanzo cha mafuriko hayo John Hyewele alisema kuwa, mvua iliyonyesha ni kubwa sana kuliko uwezo wa bwawa na hivyo kusababisha maji kupita juu na kwenda yalikoenda na kusababisha hasara hiyo.
Hivyo amewataka wakijiji kuweza kuwa na umoja katika kulitunza bwawa lao hilo liweze kuwanufaisha katika kazi zao za kilimo cha umwagiliziaji kama ilivyo.
Na kwa upande wake Diwani wa kata ya lamadi Emanuel Desera amesema kuwa anampongeza Waziri Kaman kwa kuweza kuguswa na tukio hili na kuvunja kazi zake zote na kisha kuja kuwaona wananchi wake waliokumbwa na mafuriko kijiji lamadi.
Pia Desera aliongeza kuwa wanachi wamepewa mahitaji ya muhimu ikiwemo vyakula,blanket magodoro ili waweze kujikimu kwa sasa huku wakisubili maamuzi ya serikali kuu.
Mbali na hayo Dk Kaman aliwataka wananchi wote wanaoishi katika vyonza vya maji,pembezoni mwa mito na wale waliojenga katika majaluba kuweza kuhama mara moja ili waweze kuepukana na hili janga kwani mvua bado inaendelea.
Aidha amewata wananchi wote kuwa na subra kwani matatizo yao yanashughulikiwa haraka sana na ndio maana hata mbunge wetu tuko nae katika hili.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni