Mabingwa watetezi wa kombe la ligi kuu nchini Uingereza, Manchester City wameendelea kujiweka katika wakati mgumu wa kulitwaa kombe hilo katika msimu huu, baada ya kushuhudia wakichapwa mabao 2-1 na Crystal Palace katika mchezo wa ligi kuu nchini humo uliochezwa jana.
Wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Selhurst Park, Crystal Palace wanaonolewa na kocha Alan Pardew waliwapa furaha ya jumatatu ya Pasaka mashabiki wao kwa kubakiza pointi tatu nyumbani.
Wakiwa katika nafasi ya 11 na pointi 39, Crystal Palace walijipatia bao la kwanza katika dakika ya 34 mfungaji akiwa ni Glenn Murray na Jason Puncheon akifunga bao la pili katika dakika ya 47. Bao pekee la kufutia machozi lilifungwa na Sergio Aguero katika dakika ya 77. Manchester City wapo katika nafasi ya nne wakiwa na pointi 61.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)








Hakuna maoni :
Chapisha Maoni