Mkuu wa jeshi la polisi nchini
Malawi amewaagiza polisi kuwapiga risasi wahalifu wanaoshambulia watu
wenye albinism ili kuuza viungo vyao kwa matumizi ya vitendo vya
ushirikina.
Mkuu huyo Lexen Kachama amewaambia
maafisa polisi kwamba wawapige risasi wahalifu watakao wakuta wakati
wakifanya kitendo cha utekaji watu wenye albinism.
Kwa mujibu wa Chama cha Watu Wenye
albinism nchini Malawi, albino sita wameuwawa tangu mwezi Desemba
mwaka jana hadi Aprili mwaka huu.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni