Jaji wa North Carolina ameridhia
mwanaume mmoja anayetuhumiwa kuwauwa wanafunzi watatu Waislamu nchini
Marekani, apatiwe adhabu ya kifo.
Jaji Mwandamizi Orlando Hudson
amesema kwamba waendesha mashtaka wanahoja kuu mbili za msingi
zinazomfanya mtuhumiwa huyo Craig Stephen Hicks kustahiki kukabiliwa
na adhabu ya kifo.
Craig Hicks anashtakiwa kwa mauaji
ya Deah Barakat na mkewe Yusor Mohammad Abu-Salha pamoja na dada yake
Razan Mohammad Abu-Salha.
Wanafunzi Waislamu waliouwawa wakiwa katika picha ya pamoja


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni