Waziri wa ardhi aliyesimamishwa kazi
Charity Ngilu leo anatarajiwa kukutana na maafisa wa kukabiliana na
rushwa katika jengo la Maadili Jijini Nairobi kuhojiwa kuhusiana na
tuhuma za ukiukaji wa maadili.
Bi. Ngilu, ambaye amelazimishwa
kuachia madaraka ili kupisha uchaguzi, alikuwa anatumia Sikukuu ya
Pasaka katika kujenga utetezi wake kuhusiana na tuhuma zinazomkabili.
Msemaji wa Tume ya Maadili na
Kupambana na Rushwa Kenya, Yasin Amaro, amesema kuwa pia Msajili Mkuu
wa Ardhi Kenya Sarah Mwendwa naye pia ayafika mbele ya tume hiyo
kujitetea hii leo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni