Kaburi linalohisiwa kuzikwa watu
wengi hadi kufikia 1,700 limebainika katika mji wa Tikrit nchini Irak
uliotwaliwa kutoka kwa kundi la Dola ya Kiislam (IS).
Eneo hilo lipo karibu na iliyokuwa
kambi ya Marekani ya Camp Speicher katika mji wa Tikrit.
Wachunguzi wa matukio ya vifo wa
Irak wameanza kufukua na kuhamisha makaburi 12 katika mji huo ambao
hivi karibuni umekombolewa kutoka kwa IS.
Mwezi Juni mwaka 2014 kundi la IS
linalojulikana kwa vitendo vya ukatili lilituma picha za video kwenye
tovuti likionyesha likiwauwa wanajeshi, wengi wakiwa ni waumini wa
dhehebu la Shia.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni