Baadhi ya nyumba zikiwa zimeanguka kijiji cha Lamadi kutoka na mvua kubwa iliyosababisha mafuriko.
Habari, picha na Shushu Joel,Busega.
Wananchi waliokumbwa na maafa ya mafuriko yaliyosababisha nyumba zao kubomoka wameiomba serikali kuwapelekea chakula pamoja na mablanketi na Mahema ili kuweza kujinusuru na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo.
Wakizungumza na Rweyunga Blog, wananchi hao wamesema kuwa mpaka sasa misaada iliyotolewa kwa waathirika hao ni michache ukilinganisha na mahitaji kwani wengi wao hawana hata chakula kutokana na kusombwa na maji.
Mmoja wa waathirika wa maafa hayo Pendo Amosi alisema kuwa mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali ilianza juzi kunyesha majira ya saa sita usiku hali ambayo iliyosababisha nyumba kuanza kubomoka.
Alibainisha kuwa baada ya kuona maji yanajaa kwenye nyumba, baadhi ya wananchi walianza kukimbilia kwenye majengo ya shule ya msingi Nyamajeshi kwa ajili ya kuweza kupata sehemu iliyosalama .
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Gaudencia Bamugileki alisema kuwa Vitongoji vilivyoathirika na mafuriko ni pamoja na kitongoji cha kisesa,iseni B,sokoni,Lukungu,mwalukonge na Kijiji cha Lamadi.

“Kamati ya maafa wilaya imeshaanza kufanya tathimini ili kuweza kujua ni watu wangapi wamekumbwa na maafa hapa tupo na wataalamu kwa kushirikiana na wenyeviti wa vitongoji kubaini ni watu gani wameathirika na mvua hiyo”Alisea Bamugileki.
Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya mifugo na uvuvi Dkt,Titus Kamani akiongea kwa njia ya simu na wandishi wa habari waliofika katika maafa hayo alisema kuwa hilo ni janga la kitaifa hivyo hivyo amewapa le wananchi walioathirika na tukio hilo na ameahidi kuwasaidia wahanga waliokubwa na maafa hayo.
Mbunge huyo alitoa pole na kuwapa msaada wa dharula wa Unga wa mahindi tani 1.25 zenye mifuko ya ujazo kilogramu 25,Maji ya kunywa katoni 30 na Mablanketi 50 kwa ajili ya kuwapatia wahanga wa mafuriko hayo.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa kwa wananchi wangu nimetoa msaada kidogo kwa ajili ya kuwasaidia walioathirika na mafuriko na tutaendelea kutoa msaada zaidi na mpaka sasa ninasubili tathimini ifanyike ili tuweze kujua ni kaya ngapi zimeathirika na wanahitaji msaada”Alisema Kamani
Pia mbunge huyo amewaomba watumishi wa serikali kusimamia misaada inayotolewa ili kuweza kuwafikia walengwa husika
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni