Mchezo huo ulichezwa usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Vicente Calderon, ambao ni uwanja wa nyumbani wa Atletico Madrid ulishuhudia soka safi toka kwa timu zote mbili zenye upinzani wa jadi.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akiruka juu kupiga kichwa mpira wakati wa mchezo huo uliomalizika kwa kutofungana. Mchezo huo ulikuwa na msisimko mkubwa kwa wachezaji, makocha na mashabiki wa timu zote mbili, kwani timu hizo ndizo zilizocheza fainali ya kombe hilo mwaka jana mjini Lisbon nchini Ureno, ambapo Real Madrid walilitwaa kombe hilo baada ya kuishinda Atletico kwa mabao 4-1. Timu hizo zitarudiana katika uwanja wa nyumbani wa Real Madrid.








Hakuna maoni :
Chapisha Maoni