.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 15 Aprili 2015

VIONGOZI WA COASTAL UNION WATAKIWA KUSHIKAMANA


VIONGOZI wa Klabu ya Coastal Union wamewatakiwa kushikamana vilivyo
ili kuweza kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika michezo yao iliyosalia katika Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania Bara.

Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Magalula Saidi wakati
alipokutana na viongozi wa timu hiyo ofisini kwa lengo la kufahamiana
ambapo Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto aliwaongozwa
viongozi wengine kwenye kikao hicho.

Alisema kuwa muda uliobakia kwenye mechi za Ligi kuu sio wa kuanza
kufikiria ni kitu gani kimetokea bali ni kuweka mipango imara na madhubuti itakayowapa mafanikio ili waweze kujipanga msimu ujao kwa ligi nyengine.

Aidha aliwataka viongozi hao kujiepusha na migogoro, mifarakano iliyokuwa na tija kwani hali hiyo ikiruhusiwa itashindwa kuwapa maendeleo na kukwamisha mipango yao waliojiwekea.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto
alimuhaidi mkuu wa mkoa huyo kuyafanyia kazi kwa asilimia kubwa maelekezo aliyoyatoa ili waweze kupata mafanikio..

Naye, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Coastal Union, Akida Machai alisema changamoto zilizojitokeza kwenye michuano hiyo watazifanyia kazi kwa umakini mkubwa ili ziweze kuleta ufanisi katika michezo iliyosalia.

Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa soka akiwemo Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho la soka Nchini (TFF) Khalid Abdallah.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni