.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 16 Aprili 2015

LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA HATUA YA ROBO FAINALI, PSG YATANDIKWA 3-1 NA FC BARCELONA

 Wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani jijini Paris, timu ya soka ya Paris Saint Germain ( PSG ) usiku wa kuamkia leo wamekiona cha moto baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 toka kwa FC Barcelona toka Hispania katika mchezo wa robo fainali wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Mabao mawili toka kwa mshambuliaji Luis Suarez raia wa Uruguay katika dakika za 67 na 79 na bao la kuongoza lililowekwa kimiani katika dakika ya 18 na mshambuliaji Neymar yalitosha kuwapa Barcelona nafasi nzuri ya kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo, kwani katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Camp Nou, Barcelona watahitaji sare yoyote ili kusonga mbele.
Wachezaji wa FC Barcelona wakimpongeza mwenzao, Luis Suarez aliyelala chini baada ya kufunga goli.








Hakuna maoni :

Chapisha Maoni