.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 21 Aprili 2015

MAELFU YA RAIA WAPYA WA TANZANIA WAPEWA VYETI VYAO KATIKA MAKAZI YA MISHAMO, MPANDA

Afisa Operesheni wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Stephen Daniel (kushoto) akiwaelekeza raia wapya wa Tanzania katika Kijiji cha Ilangu, Makazi ya Mishamo, kuwasilisha vyeti vya kliniki vya watoto wao ili waweze watoto wao kuwekwa kwenye kumbukumbu ya Serikali. Watoto wote waliozaliwa baada ya mwaka 2010 ni raia wa Tanzania wa kuzaliwa, hivyo hawatapewa vyeti vya uraia kama wanavyopewa wazazi wao. Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania. Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Mkuu wa Makazi ya Mishamo, Fredrick Nisajile (kulia) akiwapanga watoto wa Kijiji cha Ilangu katika makazi hayo yaliyopo wilayani Mpanda Vijijini, ili watoto hao pamoja na wazazi wao waweze kupewa vyeti vya uraia. Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania. Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni