Kuingia kwa bao la mapema la Man City, kuliwaamsha Mashetani hao wekundu na kuanza kujibu mapigo na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 14 mfungaji akiwa ni Ashley Young. Dakika chache baadaye
Marouane Fellaini akaifungia Manchester United bao la pili katika dakika ya 28.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Man United kufanikiwa kupata bao la tatu mfungaji akiwa ni Juan Mata katika dakika ya 67 na bao la nne nala ushindi likifungwa na Smalling katika dakika ya 73.
Bao la pili la Manchester City lilifungwa tena na Aguero katika dakika ya 89.
Kwa matokeo hayo, Manchester United wamefikisha pointi 65 wakiwa nafasi ya tatu huku mabingwa watetezi wa kombe hilo, Manchester City wakiwa na pointi 61 wakiwa nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu Uingereza inayoongozwa na Chelsea yenye pointi 73.









Hakuna maoni :
Chapisha Maoni