.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 11 Aprili 2015

MATUKIO MBALIMBALI YA BALOZI SEIF ALIPOFUNGUA MKUTANO WA 31 WA ALAT JIJINI DAR ES SALAAM


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiingia ndani ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere Jijini Dar es salaam kuufungua Mkutano wa 31 wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania kwa niaba ya Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.Kulia yake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Hawa Abdulrahman Ghasia na aliyeko nyuma ya Balozi ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa ambae pia ni Meya wa Jiji la Dar es salaam Dr. Didas Massaburi.
Balozi Seif akipatiwa maelezo ya jinsi Idara ya Bohari Kuu ya Taifa Tanzania inavyotekeleza majukumu yake kutoka kwa Meneja wa Taasisi hiyo Daudi Msasi wakati alipotembelea maonyesho kabla ya kuufungua Mkutano wa 31 wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa.
Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki wa Benki ya NMB Bibi Domina Ferouz wa pili kutoka Kulia akimuelezea Balozi Seif mafanikio makubwa iliyoipata Benki hiyo katika kusaidia huduma za Kijamii Nchini Tanzania. Kulia ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa ALAT ambae pia ni Meya wa Jiji la Dar es salaam Dr. Didas Massaburi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Hawa Abdulrahman Ghasia.
Balozi Seif akiufungua Mkutano wa 31 wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania { ALAT } kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere Jijini Dar es salaam.
Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Jumiya ya Serikali za Mitaa Dr. Didas Mssaburi akilizindua rasmi Jarida la Jumuiya hiyo pamoja na Kitabu cha Utafiti.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 31 wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa kutoka Halmashauri mbali mbali Nchini Tanzania wakiwa katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano huo uliofanywa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwa Niaba ya Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 31 wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa kutoka Halmashauri mbali mbali Nchini Tanzania wakiwa katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano huo uliofanywa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwa Niaba ya Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.

                                                                         (Picha na Hassan Issa OMPR)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni