.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 6 Aprili 2015

MHE. MEMBE ATOA RAI KWA VIONGOZI WA DINI ZOTE PAMOJA SERIKALI KUHIMIZA VIJANA WAIPENDE DINI ILI KUDUMISHA AMANI, UTULIVU NA UADILIFU

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ambaye alikuwa mgeni rasmi akiongea katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka ililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015. Pembeni ni Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama.
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akiwapungia watu waliohudhuria katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015. (Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason blog).

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akishirikiana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara (kulia) na Mchungaji Mwasota kukata keki. Aanayeshudia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki.


Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akimlisha keki Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki. Pembeni anayeshuhudia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara.Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini anayefahamika kwa jina la Rebbeca Malope akitoa burudani katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mwimbaji Rose Mhando akiwasha moto wa kamata pindo la Yesu katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
                                            Mwimbaji John Lissu akitumbuiza jukwaani

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni