Wahamiaji haramu 1,500 wameokolewa
kutoka kwenye boti wakati wakijaribu kuvuka kuingia nchini Italia
katika muda wa saa 24, kwa mujibu wa kikosi cha ulinzi cha pwani ya
Italia.
Kikosi cha Jeshi la Majini pamoja na
kikosi cha ulinzi wa pwani vimewaokoa wahamiaji hao katika maeneo
matano tofauti.
Shirika la Umoja wa Mataifa la
Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limesema karibu watu 3,500 wamekufa maji
na wengine zaidi ya 200,000 wameokolewa wakijaribu kukatiza bahari ya
Mediterranean kwenda Ulaya katika mwaka jana.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni