Cristiano Ronaldo ameiongoza Real
Madrid kufanya maangamizi baada ya kufunga hat-trick ndani ya dakika
nane katika kipindi cha kwanza na kuisambaratisha Granada kwa mabao
9-1 hapo jana.
Mchezaji huyo raia wa Ureno
alipachika kimiani tena mabao mawili katika kipindi cha pili na
kutimiza kufunga magoli matano peke yake katika mchezo huo wa ligi
kuu ya Hispania. La Liga.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye
dimba la Santiago Bernabeu, mshambuliaji wa Real, Karim Benzema
alipachika wavuni mabao mawili, huku Gareth Bale akiwa wa kwanza
kucheka na nyavu na kufungulia mvua hiyo ya magoli.
Ronaldo akimtoka beki wa Granada
Gareth Bale akipachika wavuni goli



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni