.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 10 Aprili 2015

MKUU WA MKOA SIMIYU, ERASTO MBWILO AWATEMBELEA WAATHIRIKA WA MAFURIKO


                                                                                       Na shushu Joel,Busega.

MKUU wa mkoa wa Simiyu, Elaston Mbwilo amewataka wananchi wote wanaoishi mabondeni kuhama mara moja katika maeneo hayo.

Hayo ameyasema wakati akitembelea baadhi ya vijiji Kisesa,Kalago na Lamadi vilivyopatwa na mafuriko wilayani Busega.

Mbwilo amewataka wananchi hao kuweza kuhama katika maeneo ya karibu na mito kwani hii ni hatari kubwa sana katika mazingira ya kuishi mwanadamu.

Mbali na hayo mkuu wa mkoa aliwataka wenyeviti wote wa vijiji kuweza kuwatafutia wananchi maeneo mazuri ya kuishi ili watoke kwenye maeneo ya mito na majaruba kwani huko ni chanzo cha maji.

Aliongeza kuwa kipindi hiki si cha kumtafuta nani mbaya bali haya yote ni mapenzi ya mungu kwani hakuna mtu yeyote Yule aliyekuwa anayatarajia haya kutokea, lakini tumshukuru mungu hakuna wananchi yeyote Yule aliyepoteza maisha kwa tukio hili.

Aidha mkuu wa mkoa aliwapongeza wale wote waliojitokeza kuwasaidia waathirika wote wa mafuriko hayo katika kijiji cha lamadi, na ametoa wito kwa watu wengine wote walioguswa na tukio hili kuweza kujitolea kuwasaidia watu wote waliopatwa na mafuriko wilayani humo.

Pia mkuu wa mkoa alitoa msaada wa mahindi wa chakula tani 2,maji katoni 20 na mchele kilo 200 kwa wote waliopatwa na janga hilo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha kalago Mpuya Lucas alimpongeza mkuu wa mkoa kwa moyo wake wa dhati wa kuja kuwaona waathirika wa mafuriko hayo na kutoa msaada kwao.

Mpuya aliongeza kuwa muda si mrefu watakaa na serikali ya kijiji ili waweze kutafuta maeneo kwa ajili ya kuwapatia wale wote walio mabondeni ili waweze kuhama katika maeneo hayo na wale walio kando ya mito ambako ndiko maji mengi uelekea maeneo hayo.

Kwa upande wa wananchi Susana Sabini alimpongeza mkuu wa mkoa kwa kuweza kuja kuwajulia hali waathirika hao.

Pia tunakuhakikishia kuwa tutamwambia mwenyekiti wetu wa kijiji aweze kuhakikisha wale wote tuliopatwa na mafuriko tunapatiwa maeneo ili tuweze kuhama na wale walio na maeneo wahame kabisa na huku pabaki sehemu za kulima mbunga maana ni maeneo ya mabondeni.

MWISHO.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni