Hali ya hofu miongoni mwa wananchi
wa Mkoa wa Arusha imejitokeza, leo asubuhi, kufuatia kusambaa kwa
ujumbe mfupi kwenye mitandao ya kijamii na simu za kiganjani kuwa
kuna magaidi wanne wamekamatwa na silaha aina ya SMG katika chuo cha
Uhasibu Njiro (IAA).
Akizungumzia taarifa hizo,Kamanda wa
Polisi Mkoani Arusha, Liberatus Sabasi, amesema wananchi wanapaswa
kuendelea na shughuli zao kama kawaida na kupuuza ujumbe huo.
Amesema taarifa hizo zitakuwa
zimesambazwa na wahuni wachache kwa lengo wanalojuwa wenyewe, ila
ulinzi wameimarisha kila mahali watu wafanye shughuli zao kama
kawaida.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi
Ntibenda, alipopigiwa simu ya kiganjani, amesema huo ni uwongo na
kila mmoja aupuuze.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni