Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,
John Kerry pamoja na mwenzake wa Cuba, Bruno Rodriguez wamefanya
mazungumzo ya kwanza ya ngazi ya juu baina ya nchi hizo mbili baada
ya zaidi ya nusu karne kupita.
Mawaziri hao wawili wamefanya
mazungumzo ya ndani baada ya kuwasili Jijini Panama.
Wakati huo huo idara ya serikali ya
Marekani, imeripotiwa kupendekeza nchi ya Cuba kuondolewa katika
orodha ya nchi zinazosemekana kusaidia ugaidi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni