Serikali ya Somalia imetoa ahadi ya
kutoa zawadi ya fedha kwa mtu atakayefanikisha kukamatwa kwa kati ya
viongozi 11 waandamizi wa kundi la al-Shabaab.
Katika zawadi nono hiyo ya fedha
jumla ya kiasi cha dola 250,000 zimetengwa kwa ajili mtu atakayetoa
taarifa zitakazofanikisha kukamatwa mkuu wa al-Shabaab Ahmed Diriye.
Orodha ya viongozi wengine pamoja na
majina yao ya kupachikwa imetolewa baada ya kikao cha baraza la
mawaziri ikiwa ni wiki moja baada ya shambulio la al-Shabaab katika
chuo cha Kenya.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni