Maafisa wa Carolina Kusini wametoa
video mpya inayoonyesha tukio la afisa polisi akimuua mwanaume mmoja
Mmarekani mweusi asiye na silaha kwa kumpiga risasi mgongoni.
Picha hizo zinaonyesha gari la
mwanaume huyo Walter Scott likisimamishwa na afisa wa polisi
Michael Slager na kumuomba nyaraka
za kazi.
Baada ya afisa Slager kurejea katika
gari la polisi, Scott alifungua mlango wa gari na kukimbia akiwaacha
abiria aliokuwa amewabeba ndani ya gari, ndipo alipopigwa risasi na
kufa.
Polisi Slager amekamatwa kwa kosa la
mauaji baada ya picha ya video kumuonyesha akimpiga risasi Scott
wakati akikimbia.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni