Mwanamke aliyekuwa na bunduki pamoja
na mabomu ya kurusha kwa mkono amepigwa risasi na kufa akijaribu
kufanya shambulizi katika makao makuu ya polisi nchini Uturuki, ikiwa
siku moja tu kupita baada ya kutokea utekaji katika Jiji la Instabul.
Picha ya mwanamke huyo mwenye nywele
zenye rangi nyekundu akiwa amelala chini, akiwa na bunduki pembeni
yake imeonyeshwa kwenye televisheni zinaonyesha polisi wakizingira
maeneo ya jirani ya mtaa wa Aksaray.
Tukio hilo limetokea siku moja baada
ya mwendesha mashtaka wa Uturuki, Mehmet Selim Kiraz, kutekwa
mahakamani na mtu kundi la Revolutionary People's Liberation
Party-Front (DHKP-C) na kisha kuuwawa.
Mtekaji akiwa na mwendesha mashtaka Mehmet Selim Kiraz
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni