Milio ya silaha nzito imeripotiwa
kusikika leo alfajiri katika Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya
katika shambulio lililofanywa na watu wasiojulikana.
Watu wenye silaha inasemekana
wameshambulia taasisi hiyo ya elimu leo majira ya saa 5:30 alfajiri.
Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya
limesema maafisa polisi wawili na mwanafunzi mmoja amejeruhiwa na
wamekimbizwa hospitali. Vikosi vya Jeshi la Ulinzi Kenya vimefika
katika chuo hicho.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni