Naibu Waziri wa Afya, Mh Stephen Kebwe akiwasalimia wagonjwa hospitali ya Bwagala-Turiani. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero, Mh Amos Makalla.
Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero, Mh Amos Makalla jana amechangiwa fedha kiasi cha sh 2,319,500 na wananchi wa kijiji cha Manyinga na vijiji vya jirani kwa ajili ya kuchukua fomu ya ubunge mara muda utakapofika.
Tukio la kuchangiwa fedha za kuchukulia fomu lilichagizwa na Naibu Waziri wa Afya Dr Stephen Kebwe aliyefanya ziara ya kukagua hospitali teule ya Bwagala na kisha kuongea na wananchi kwenye mkutano mkubwa wa hadhara.
Alipopanda jukwaani, Dr Stephen Kebwe alisema, ninavyo waona mna furaha sana na mnampenda sana mbunge wenu, wananchi wakamjibu kwa sauti " Makalla ni jembeee ".
Kusikia hivyo Dr Kebwe akawatania kama kweli mnampenda Amos Makalla basi onyesheni kwa kumchangia fomu, hapo ndipo umati ulipolipuka na kuanza kuwasilisha michango na kadri watu walivyozidi kuchangia Dr Kebwe naye alichangia dola za kimarekani Mia moja.
Akiwashukuru wananchi hao, Mbunge wa Mvomero alisema amepokea msaada huo kwa heshima kubwa na kwa maana kubwa ikiwepo imani kubwa walioonyesha kwananchi hao kwake.
Amewaaidi kugombea tena ubunge na zaidi amewaomba ushirikiano na amewahakikishia utumishi uliotukuka.
Aidha katika tukio lingine, amewakabidhi Wawakuda Saccos ya Kijiji cha Dakawa msaada wa computer na printer yenye thamani ya sh 2,000,000 .
Akishukuru mwenyekiti wa Wawakuda Saccos ndugu Mohamed Mkupete, alimshukuru sana mbunge kwa msaada wa computer ambayo walimuomba wiki moja iliyopita na leo ametembelea,
"mheshimiwa Makalla wewe ni mtu makini na huna longolongo ndani ya wiki moja umetekeleza tunakushukuru sana".
Wananchi wakichanga hela kwa ajili ya kumkabidhi Mbunge wao, Mh Amos Makalla achukulie fomu za kuwania tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni