.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 4 Aprili 2015

NGUMI KUFANYIKA MKWAKWANI TANGA MEI 2

Bondia Alen Kamote wa Tanga atapanda ulingoni mei 2 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga kukabiliana na Emilio Norfat katika mpambano wa raundi 12.

Siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mengine makali, na moja ya mpambano wenye mvuto zaidi ni kati ya bondia mwenye makazi yake mkoa wa Morogoro Cosmas Cheka atakaekabiliana na Said Mundi kutoa mkoa wa tanga

Promota wa mpambano huo Ally Mwazoa aliongeza kwa kusema mbali na mapambano hayo kutakuwa na mapambano mengine yatakayowakutanisha Jacobo Maganga na Fadhili Kea wakati Juma Mustafa akipamana na Ally Magoma uku Saimon Zabroni akioneshana umwamba na Hamisi Mwakinyo na Jumanne Mohamed na Bakari Shendekwa na Zuber Kitandura na Rajabu Mahoja

Mpambano uho unafanyika mkoa wa tanga baada ya kutopata burudani ya mchezo wa masumbwi kwa kipindi cha mda mrefu kidongo hivyo mpambano uho utafuraiwa na wakati wa Tanga na vitongoji vyake


Siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali

Na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni