.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 27 Aprili 2015

RAIS DR. JAKAYA KIKWETE AONGOZA WATANZANIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA MUUNGANO

1
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dr.Jakaya Kikwete akikagua gwaride la Heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania ulioasisiwa na Wazee wetu Mwalimu J.K.Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume mwaka 1964 kwa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar, Dr. Jakaya kikwete ameongoza maelefu ya watanzania kwenye uwanja wa Taifa katika sherehe za kuadhimisha muungano huo sherehe zilizohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, Vyama vya Siasa, viongozi wa dini na wananchi wageni waalikwa kwa ujumula.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-UWANJA WA TAIFA-DAR ES SALAAM) 2 
Vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama vikiwa vimejipanga katika gwaride 6 
Rais Jakaya Kikwete akirejea jukwaa kuu mara baada ya kukagua gwaride la Heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Taifa. 7
Viongozi mbalimbali wa serikali wakiwa wamesimama kwenye jukwaa kuu kwa ajili ya kumpokea Rais Dr. Jakaya Kikwete. 
8 
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda mara baada ya kukagua gwaride la Heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania. 9 
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mh. Pandu Ameri Kificho Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar mara baara ya kukagua gwaride la Heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania. 10 
Rais Jakaya Kikwete akiakizungumza jambo na Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein huku Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiwaangalia kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na kulia ni Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal. wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania 12 
Rais Jakaya Kikwete akipokea heshima kutoka Vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.
 13Mwenyekiti wa Chama cha TLP Taifa na Mbunge wa jimbo la Vunjo Mh. Augustino Lyatonga Mrema akiwa ameungana na wageni wengine waalikwa katika maadhimisho ya sherehe hizo. 14
Kikosi Cha bendera kikitoa heshima zake Mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dr. Jakaya Kikwete wakati wa maadhimisho hayo.  15
Vikosi vya ulinzi na usalama vikipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Mh Dr. Jakaya Kikwete. 16
Kikosi cha Mizinga kikipita na kutoa heshima zake 17
Kikosi cha wanamaji wanawake kikipita 18
Kikosi maalum cha walinzi wa viongozi kikipita na kutoa heshima. 19
Kikosi maalum cha mizinga ya kutungulia ndege kikitoa heshima zake 20
Kikosi maalum cha Makomandoo kikitoa heshima zake 21
Kikosi cha makomandoo wana maji kikipita na kutoa heshima. 22
Kikosi cha FFU kikipita  23
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo. 24
Baadhi ya viongozi wakiwa katika sherehe hizo. 25
                              Wananchi mbalimbali wakiwa katika maadhimisho hayo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni