Rais Barack Obama amesema mkutano
wake na rais wa Cuba, Raul Castro utasaidia nchi zao mbili kubadili
mitazamo yao baada ya kupita miongo kadhaa ya hali ya uhasama.
Obama ameelezea mkutano huo baina ya
mataifa hayo ya Amerika ni wa kuaminiana na wenye mafanikio.
Amesema kuwa mataifa hasimu ya
Marekani yanaweza kuendelea na tofauti zao, lakini kutokuwa na
maendeleo katika makubaliano ya masuala yenye maslahi yanayofanana.
Mkutano huo ni wakwanza rasmi kwa
viongozi wa mataifa hayo kufanyika baada ya kupita karibu zaidi ya
nusu karne.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni