Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani
Papa Francis ametumia neno mauaji ya kimbari, wakati akielezea mauaji
ya wa Armenia wengi chini ya utawala wa Ottoman wakati wa vita ya
kwanza ya dunia miaka 100 iliyopita.
Matamshi hayo ya Papa ameyatoa
wakati wa misa Jijini Vatican, ambapo wa Armenia pamoja wanahistoria
wanasema watu milioni 1.5 waliuwawa na vikosi vya Ottoman mnamo mwaka
1915.
Hata hivyo kauli hiyo ya Papa
Francis inatarajia kuibua hasira za taifa la Uturuki, ambalo limekuwa
likisisitiza kuwa mauaji hayo hayakuwa ya kimbari.
Rais wa Armenia Serzh Sargsyan
alihudhuria misa hiyo iliyofanyika Vatican, katika kumbukumbu ya
karne ya 10 ya mauaji hayo ya wa Armenia.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni